Waziri Kagwe azindua baraza la kupambana na Malaria

Waziri wa afya Mutahi Kagwe Picha kwa Hisani

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amezindua baraza la kupambana na ugonjwa wa Malaria ifikapo ruwaza 2030.

Kagwe amesema baraza hilo litahahakikisha msambao wa ugonjwa huo unakamilika hususan kwenye Kaunti za Siaya na Busia ambapo vifo vinavyotokana na Malaria vinaongezeka.

Akizungumza na vyombo vya habari,Kagwe amesema kuwa wizara yake imepatiana neti zilizopuliziwa dawa pamoja na dawa za kudhibiti Malaria miongoni mwa bidha zingine kwa wakenya hususan wamama wajawazito.

Aidha ameelezea kuwa ipo changamoto ya kupata vifaa vya afya kwa wakati haswa vifaa vya kupima ugonjwa wa Malaria ikizingatiwa kuwa vifaa hivyo huagizwa kutoka nje ya nchi.

Ametoa wito kwa wadau kufanya kazi pamoja na kuhakikisha bidhaa hizo zinatengenezwa nchini akieleza kuwa  hatua hiyo itainua sekta ya viwanda nchini,kutenga nafasi za kazi,kuhakikisha bidhaa hizo zinapatikana kwa urahisi na kwa wakati ufaao pamoja na kupunguza kutegemea nchini za nje kutuletea bidhaa hizo muhimu za kusaidia vita dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Kagwe amedokeza kuwa ugonjwa wa Malaria unapunguza kukuwa kwa uchumi kwa asilimia 1.3 kila mwaka na wafanyikazi hukosa takribani siku 12 za kufanya kazi kila mwaka kwa sababu ya malaria.

Vilevile,malaria hupunguza viwango vya masomo na kufanya watoto kukosa asilimia 3 ya masomo yao.

Aidha,waziri Kagwe ameeleza kuwa ili kufaulu kwa vita dhidi ya Malaria pengo la Ksh 24b litatuliwe ndiposa utekelezwaji wa mpango mkakati wa kupambana na ugonjwa wa malaria wa kati ya mwaka wa 2019 hadi 2023 ufanyike.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *