Kaimu Jaji Mkuu afungua kongamano la majaji Mombasa

Kaimu Jaji mkuu Philomena Mwilu Picha kwa Hisani
Kaimu jaji mkuu Philomena Mwilu amefungua rasmi kongamano la majaji wa mahakama kuu kutoka pwani ya Kenya kwa lengo la kuimarisha utendakazi wa idara ya mahakama msimu huu wa janga la corona.
kuhusu mabadiliko kwenye idara ya mahakama imebainika kesi 58,487 kwa zaidi ya miaka tano zingali kuamuliwa,aidha tangu mwaka wa 2017 hadi Desemba 2020,kesi 70,453 zimeamuliwa huku kesi 6,995 ambayo ni sawia na asilimia 88 zingali kuamuliwa kwa zaidi ya miaka 5 sasa.
Mwilu amechukua nafasi hiyo kuwapongeza majaji kwa kuamua kesi za uhalifu ambapo hadi Agosti 20,2019 kiwango cha kuamua kesi za uhalifu ilikuwa 84.6, kiwango hicho kikiimarika hadi asilimia 112 na kupita kiwango walichotarajia cha asilimia 97.5 ambayo ni zaidi ya asilimia tajika akieleza kuimarika kwa viwango vya kutoa haki kwa wakenya.
Hata hivyo suala la mrundiko wa kesi mahakamani ingali changamoto kulingana na jaji huyo, mwezi Juni 2020 kulikuwa na kesi 89,415 ambazo bado hazikuwa zimeamuliwa katika mahakama kuu idadi hiyo ikiongezeka hadi 92,530 kufikia Desemba 2020.
Kaimu jaji mkuu huyo amewahimiza majaji kutumia rasilimali zilizopo kwenye utendakazi wao katika kukabiliana na upungufu wa fedha,halkadhalika matumizi ya teknolojia wakati huu wa janga la corona huku afisi ya msajili kwenye idara ya mahakama ikihimizwa kubuni mbinu zitakazokabiliana na majanga katika idara hiyo .
.