Mashirika yataka hospitali ya Tudor kutotengewa wagonjwa wa corona

Hatua ya serikali ya kaunti ya Mombasa kutenga hosipitali ya kaunti ndogo ya Tudor kama kituo cha kuwahudumiya wagonjwa walioambukizwa virusi vya corona imezua mdahalo miongoni mwa wateja wanaopata huduma kutoka kwa hosipitali hiyo.

Mashirika kadhaa yasiyo kuwa ya serikali ikiwemo shirika linalotetea waathiriwa wa dawa za kulevya miongoni mwa mashirika mengine wametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Mombasa kutotenga hospitali ya Tudor kwani watakosa huduma muhimu kama kupata ushauri wa afya ya akili,pamoja na kusaidia waathiriwa wa dhulma za kijinsia kutoka hospitali hiyo.

Wakiongozwa na Anne Nyambura ,wamesema huenda waathiriwa wa visa vya dhulma za kijinsia wakose kupokea fomu ya P3 pamoja na visa hivyo kukosa kurekodiwa hospitalini hali itakayolemaza vita dhidi ya dhulma za kijinsia .

Kadhalika wamedai  hospitali hiyo kwa sasa inapeana huduma kwa wamama wajawazito, wagonjwa wa Kifua kikuu,na wale walioambukizwa virusi vya UKIMWI.

Kundi hilo  limetaka serikali ya kaunti ya Mombasa kuweka hema au kontena kwenye hospitali hizo ambapo watapokea huduma hizo wakisema itakuwa ghali kwao kusafiri kwenda hospitali nyingine kupata huduma hizo.

Halkadhalika,Dorcas Kavita anayefanya na shirika lisilokuwa la serikali la CHEC anahofia huenda visa vya  mimba za mapema miongoni mwa vijana vitaongezeka kwani vijana watakosa huduma za upangaji uzazi pamoja na mipira ya kinga kutoka kwa hospitali hiyo.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *