Wafanyakazi Wa Sekta ya Utalii Ukanda Wa Pwani Kupokea Chanjo

Shughuli ya utoaji chanjo dhidi ya virusi vya korona kwa wafanyikazi takriban 1,800 wa sekta ya utalii na hoteli ukanda wa Pwani umeanza rasmi leo katika hospitali ya Tudor hapa Mombasa.

Kulingana na Sam Ikwaye  ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa muungano wa wafanyakazi wa hoteli KAHKC, shughuli hiyo itasaidia kuinua viwango vya utalii ukanda wa Pwani baada ya sekta hiyo kuathirika pakubwa na ujio wa covid-19.

“Tunatazamia biashara kurudi kuanzia mwezi wa saba wakati shughuli ya utoaji chanjo itakamilika.Itakuwa jambo zuri kwa wafanyakazi wa sekta ya utalii kutoka kaunti ya Mombasa kukaribisha wageni,” akasema Ikwaye.

Ikwaye ameeleza matumaini yake kuwa idadi ya wafanyakazi wanaojisajili itaongezeka kwa siku zijazo huku akishukuru serikali ya kaunti ya Mombasa na wizara ya utalii kwa kuweka sekta ya utalii mbele katika shughuli ya utoaji chanjo.

“Tunashukuru sana serikali ya kaunti ya Mombasa kwa kutambua sekta ya utalii na hoteli.Imekuwa muhimu kwa wafanyakazi hawa kupokea chanjo,”akasema Ikwaye.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *