Busia na West Pokot wapitisha mswada wa BBI

Bunge la kaunti ya West Pokot Picha kwa hisani

Kaunti za Busia na West Pokot zimekuwa miongoni mwa kaunti 5 kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020.


kwenye Kaunti ya Busia, wawakilishi wadi 53 wamepitisha mswada huo kwa pamoja isipokuwa mwakilishi wa wadi mteule Benard Odako kutoka Budalangi huku zoezi hilo likiongozwa na spika Benard Wamalwa.


Akizungumza baaada ya kupitishwa mswada huo, Spika Wamalwa amesema kuwa bunge la kaunti hiyo limeshafanya jukumu lake na sasa ni kwa wananchi kuamua kuipitisha kwenye kura ya maamuzi.


Kamati ya haki na Sheria katika kaunti hiyo ilianda vikao vya kukusanya maoni kuhusu mswada huo katika maeneo bunge ya Nambale,Matayos,Budalangi,Teso South na Teso North.


Spika huyo anatarajiwa kuwasilisha mswada huo kwa spika wa seneti Ken Lusaka.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *