Mzee Simeon Nyachae azikwa Kisii

Waziri wa zamani Simeon Nyachae Picha kwa Hisani

Rais Uhuru Kenyatta ameongoza taifa katika mazishi ya mwenda zake waziri wa zamani Simeon Nyachae katika uwanja wa Gusii,Kisii hafla iliohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo naibu rais Dr. Wiliiam Ruto.

Kenyatta amemtaja Nyachae kama mtu mwenye heshima,hekima na uadilifu ambaye utendakazi wake uliwavutia wakenya.Rais alieleza kuwa aliyofanya ni ya kupigiwa mfano na kwa kumbukumbu yake uwanja wa Gusii utabadilisha na kuitwa uwanja Simeon Nyachae.

Serikali ya kaunti ya Kisii utakabidhiwa ksh 150m ili kukarabati uwanja huo na kuuweka kwenya viwango vya kimataifa. Rais pia amemwelekeza waziri wa michezo na turathi za kitaifa Amina Muhamed kujenga akademia  ya spoti katika uwanja wa Nyantragu ambayo baadaye itaitwa aKademia ya spoti ya Nyantika-Mayoro.

Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla wametoa rambirambi zao na kumbukumbu zao wakiwa na mzee Nyachae, kinara wa ODM Raila Odinga akisifia utendakazi wake katika sekta ya umma na serikalini.

“Mzee Nyachae alikuwa katibu mkuu serikalini lakini hakujigamba, ulihisi tu.Kuna watu wengine Kenya hii lazima watukumbushe vyeo vyao ‘mimi ni waziri…mimi ni gavana,’ akasema Musalia Mudavadi.

Gideon Moi naye amesema, “Nyachae alikuwa mtu mzuri,mtiifu,mwerevu na mwenye malengo. Kama kuna kitu unaeza jifunza kutoka kwake ili kufanikiwa kwenye kwenye taaluma yako,kibinafsi na kibiashara,si lazima uibe,si lazima utumie njia za mkato.”

Familia ya mwendazake imemmiminia sifa kedede kama ngao ya familia hiyo,na mtu mcha Mungu wengi wakieleza kumbukumbu walizokuwa nazo za mzee Nyachae walipotangamana naye. Mwanae Charles Nyachae ameeleza kuwa ilikuwa uchungu kumwona babake akiwa mgonjwa nyakati za mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *