Hospitali ya rufaa na mafunzo ya mkoa wa Pwani yafaidika na mashine ya kuzalisha maji safi

Hospitali ya rufaa na mafunzo ya mkoa wa Pwani CGTRH imepata msaada wa mashine ya sola kutoka serikali ya ujerumani itakayosafisha maji ya chumvi kwa matumizi ya kunywa kama hatua ya kukabiliana na janga la Korona.

Mashine hiyo kutoka kampuni ya Boreal Light and WaterKiosk ina uwezo wa kuzalisha lita 6,000 ya maji safi ya kunywa kwa kila saa kwa saa 12  pia yaweza tumia umeme usiku wakati ambapo hakuna nishati ya jua.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi huo kwenye hospitali hiyo, afisa mkuu mtendaji na mwazilishi wa kampuni hiyo Dkt. Hamed Beheshti amesema mashine hiyo ni ya aina yake na itasaidia kuboresha viwango vya hospitali hiyo pamoja na kusaidia wagonjwa na wahudumu wa afya.

“Hebu fikiria kama mtu atatumia lita 40 ya maji haya kwa siku, hospitali hii itahudumia takribani watu 2,000 mchana kila siku kwa kutumia miale ya jua na watu 5,000 usiku,” akasema Dkt Beheshti.

Dkt Beheshti amesema mashine hiyo itakuwa rahisi kuidumisha na kutumia na kuwa haitakuwa ghali kwa hospitali hiyo kupata maji safi ikizingatiwa kuwa eneo hilo lina maji ya chumvi ya kusafishwa.

Kwa upande wake Naibu afisa mkuu mtendaji wa hospitali ya CGTRH Mary Achola amepongeza serikali ya Ujerumani kwa mradi huo akisema utapunguza gharama ya umeme ya hospitali hiyo na badala yake fedha kuelekezwa shughuli zengine za hospitali kama kununua barakoa miongoni mwa huduma zingine.

Waziri wa mazingira katika kaunti ya Mombasa Geofrey Neto amesifia mradi huo akisema itasaidia kusuluhisha tatizo la maji safi kwenye hospitali hiyo.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *