Katibu mwandamizi katika wizara ya mawasiliano na vijana awarai vijana kujisajili na mradi wa KYEOP

Katibu Mwandamizi katika wizara ya mawasiliano na vijana Nadia Ahmed

Katibu mwandamizi katika wizara ya mawasiliano,vijana na uvumbuzi Nadia Ahmed ameeleza kuridhishwa kwake namna mradi wa kubuni nafasi za kazi kwa vijana KYEOP umepokelewa katika ukanda wa Pwani.

Mradi huo ambao uko kwenye awamu ya sita hivi sasa unanuia kufunza vijana ujuzi za maisha,jinsi watakavyojiendeleza na kujijenga kibiashara pamoja na namna ya kuwasiliana na wanaokutana nao kwenye kazi zao.

Baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo, vijana wanapata nafasi ya kuchukuliwa na kampuni inayowapa mafunzo au biashara zao kupokezwa mikopo ya kuziendeleza.

Hata hivyo, katibu huyo ameeleza kutoridhishwa na idadi ndogo ya vijana wanaojitokeza kujisajili kwenye mradi huo .

Akizungumza kwenye kikao kilichowaleta pamoja maafisa wa mawasiliano,wale wa KYEOP pamoja na maafisa kutoka hazina ya fedha za vijana na kina mama kujadili njia za kuendeleza mradi huo mbele, Bi Ahmed amewataka vijana kuzingatia maadili na kujivunia nchi yao ili miradi kama KYEOP iendelee.

Aidha, ameeleza ipo changamoto ya vijana kurudisha fedha za mikopo wanazokabidiwa.

“Kuna ugumu kwa vijana kulipa mikopo. Ni mujibu wa vijana kuelewa kuwa kuna vijana wengine nyuma yao wanaotegemea fedha hizo hivyo ni muhimu kwao kulipa,” akasema Bi Nadia Ahmed.

Vilevile,katibu huyo amedokeza kwamba ipo mipango ya kuendeleza mradi wa KYEOP kwenye kaunti zengine nchini mbali na zile 17 za sasa pindi baada ya kuasisi mradi huo ifikapo awamu ya 9 na ya mwisho wa mradi huo.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *