Kauli ya Rais yapongezwa

Kutoka Kushoto, Mwanachama wa KEMNAC Shahame Mwaringa,Mwenyekiti Sheikh Juma Ngao na Mwanachama Juma Abdulrazak katika hoteli ya Panaroma Picha kwa Hisani

Huku kauli ya rais mwisho wa wiki katika mazishi ya Mama Hannah Mudavadi aliyosema kuwa ni wakati mwafaka wa kuachia makabila mengine kuongoza Kenya zikiendelea kuibua hisia mseto,Baraza la kitaifa la ushauri kwa Waislamu nchini Kenya KEMNAC imepaza sauti ikipongeza kauli hiyo ya rais na kusema kuwa rais hakuwa mkabila akiyasema maneno hayo.

Kupitia kwa mwenyekiti wao wa Kitaifa Sheikh Juma Ngao,baraza hilo limesema kuwa kiti cha urais hakifai kuwa cha utawala wa jamii mbili na kwamba wakati umefika wa jamii zingine kuongoza nchi hii.

Baraza hilo limewarai waislamu kuunga mkono mchakato wa BBI na kupuzilia mbali viongozi wanaoipinga BBI huku akiwataka wakenya wote kudumisha amani kampeni za BBI zitakapong’oa nanga.

“Italeta faida kubwa kwa wakenya (BBI).Naomba wakenya waipigie kura kwani italeta amani nchini,” akasema Sheikh Juma Ngao.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *