Allan Wanga astaafu soka ya Kimataifa

.

Baada ya kocha mkuu wa Harambee stars Sabastian Migne kumwacha nje ya kikosi kilichowakilisha Kenya katika mashindano ya AFCON nchini Misri mshambuliaji wa Harambee stars Allan Watende Wanga amestaafu rasmi kutoka soka ya kimataifa.

Kupitia kwa barua aliyoiweka kwenye mitandao yake ya kijamii mchezaji huyo ambaye pia ni afisa wa spoti katika kaunti ya Kakamega alisema kuwa aliwakilisha nchi kwa ujuzi na ubora wake wote.

“Kwa ushirikiano wa timu,uongozi na Mashabiki kwa jumla nafikiri nimewakilisha nchi kwa ujuzi na ubora wangu wote,” sehemu ya barua hiyo inanukuu.

“Sasa ni wakati wakuwachia wachezaji wengine ambao naamini wataendeleza safari ya Harambee stars kama vile naamini nilifanya,” barua inaelezea.

Wanga aliongeza na kusema kuwa kujiondoa kwake kutoka soka ya kimataifa itampa nafasi ya kuiwakirisha klabu yake ya Kakamega Homeboyz .

Katika historia yake ya kusakata Soka Allan Wanga alianza kucheza akiwa shule ya msingi kule Kisumu kisha shule ya upili ya mtakatifu Paulo na baadae kujiunga na Lolwe FC iliyoshiriki ligi ya daraja la pili mwaka 2005 hapa nchini.

Klabu ya Tusker walimsajiri Wanga mwaka 2007 na mwaka huo wakabeba ligi ,Wanga akiwafungia mabao 21 msimu huo.

Mwaka wa 2007 Wanga aliichezea Harambee stars mchuano wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Nijeria wakipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.Allan Wanga ameifungia Harambee stars jumla ya mabao 22.

Bao lake la kwanza kufunga akicheza kama mshambulizi wa timu ya taifa ni kati ya mechi ya Kenya na Tanzania,Mechi ambayo iliisha 2-1 kwa faida ya Taifa stars ya Tanzania.

Mshambulizi huyo pia amewahi chezea vilabu mbalimbali nje ya nchi ikiwemo Petro Atletico ya Angola na FC Baku ya Azerbaijan zote akisizaidia kubeba ligi wakati huo.

Klabu ya Al-merikh ya Sudan ilimsajiri Wanga kutoka AFC Leopards mwaka 2014 Juni kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu kisha kuelekea Azam FC inayoshiriki ligi kuu nchini Tanzania baada ya mkataba wake na Al-merikh kuisha na kuwafungia mabao 12 .

Aliporejea nchini, Tusker ilimsajiri tena kwa mwaka mmoja na nusu. Baada ya mkataba wake kule Tusker kuisha Allan alijiunga na klabu ya Kakamega homeboyz timu anayoichezea hadi wakati huu.

.
Imeandikwa na Adams Kinanga
adams@wessay.co.ke.

About Author

1 thought on “Allan Wanga astaafu soka ya Kimataifa

  1. Today, I went to the beach with my kids. I found a sea shell and gave it to my 4 year old daughter and said “You can hear the ocean if you put this to your ear.” She put the shell to her ear and screamed. There was a hermit crab inside and it pinched her ear. She never wants to go back! LoL I know this is totally off topic but I had to tell someone!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *