Michuano ya mabunge ya kaunti kufanyika kama ilivyoratibiwa

Wawakilishi wadi nje ya bunge la kaunti ya Mombasa baada ya mkutano kujadili michuano baina ya mabunge ya kaunti Picha Hedlight Bosibori

Katibu mkuu wa chama cha michezo cha mabunge ya Kaunti CASA Benard Omboko ameeleza matumaini yake kuwa awamu ya tatu ya michezo baina ya mabunge ya kaunti inayotarajiwa kufanyika kwenye Kaunti ya Mombasa kati ya Mei 14 hadi 23 itaendelea licha ya changamoto za kifedha inayokumba shughuli hiyo.

Omboko amewarai serikali za kaunti kulipa ada ya shughuli hiyo kwa wakati huku akisifia michuano hiyo akisema itawapa wananchi fursa ya kutangamana na wawakilishi wadi na vilevile kujua mengi kuhusu oparesheni za kaunti.

Kwa upande mwingine,Mwakilishi wadi wa Junda Raphael Bwire ameeleza kufurahishwa kwake na Mombasa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kwani itasaidia pakubwa kukuza uchumi wa kaunti hiyo. Ameeleza kaunti hiyo imejianda vilivyo kwa michezo hiyo.

“ Naomba wananchi wajitokeze, watafaidika pakubwa wakifanya biashara,” akasema Bwire.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *