Zimbabwe yapigwa marufuku ya kuwa mwenyeji wa mechi za kimataifa


Shirika la kusimamia soka bara la Afrika (CAF)limepiga marufuku viwanja vyote vya Zimbabwe kuwa mwenyeji wa mechi yoyote ya kimataifa.

Uamuzi huo uliafikiwa baada ya shirika hilo kusema kwamba viwanja Kama Bulawayos Barbourfield,Rufaro na ule wa the national sports stadium ambao uko jijini Harare viko katika hali mbaya zaidi ya kutumiwa kucheza tena.

Kupigwa marufuku kwa Zimbabwe umeilazimisha shirika la kusimamia soka nchini humo (ZIFA) kuanza mchakato wa kutafuta viwanja mbadala nchi jirani ili kuzitumia kucheza mechi zao za nyumbani.

“Tumeanza mchakato wa kutafuta viwanja mbadala katika nchi jirani kuchezea mechi zetu za nyumbani kwa michuano inayokuja,” Zifa ilisema.

Aidha, Zifa iliongeza kuwa wako mbioni kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa CAF.

“Zifa inaongea na CAF kwa mtazamo wa kukata rufaa kwa uamuzi wao.Tunaomba Ofisi inayosimamia viwanja kututumia barua ya kuvifanyia ukarabati viwanja hivyo kabla CAF kurudi kukagua viwanja hivi tena. Mara tu tutakapopata hiyo barua tutatuma kwa CAF,” Zifa iliongeza.

Zimbabwe imeratibiwa kuwa mwenyeji wa Algeria tarehe 26 mwezi wa tatu mwaka ujao katika mechi ya kufuzu kucheza kombe la mataifa la bara Afrika.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *