Di Maria aisaidia PSG kuizima Real Madrid

Wing’a matata wa klabu ya Paris saint Germain (PSG) Angel Di Maria aliisaidia timu yake kumwadhibu aliyekuwa mwajiri wake wa zamani real Madrid mabao 3-0 katika awamu ya makundi klabu bingwa bara ulaya.Mabao mawili aliyoyafunga yalitosha kuihakikishia PSG alama tatu.

PSG walifunga goli lao la kwanza dakika ya kumi na nne baada ya straika Mauro Icardi kushirikiana na Juan Bernet kumandalia pasi Di Maria aliyeitia wavuni.Di Maria aliongeza bao la pili dakika ya 33 baada ya kutiliwa pasi murwa kutoka kwa kiungo wa Kati Idris Gueye.

Thomas meunier naye alifunga la mwisho na kuihakikishia PSG ushindi wake wa kwanza katika mechi yao ya ufunguzi katika hatua ya makundi klabu bingwa bara ulaya.

Kocha Thomas Tuchel alikuwa na kazi ngumu ya kukipanga kikosi chake cha kwanza kumenyana na Real madrid kwa sababu ya kukosekana kwa washambulizi wake wa kutegemewa wakiwemo Kylian Mbappe na Edison Cavani ambao walikosa mpambano huo kwa majeraha pamoja na Neymar anayetumikia marufuku ya mechi mbili.

Real Madrid walijizatiti mchezoni lakini waliambulia patupu.Goli ya Gareth Bale lilikataliwa kwa usaidizi wa video almaarufu VAR kwa kuwa alikuwa ameunawa mpira mshambulizi huyo kabla ya kufunga bao hilo.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya mechi hiyo ,Tuchel alisema kukosekana kwa Mastaa wake watatu kuliwafanya wachezaji wengine kutulia mchezoni na kuonyesha mchezo wao.

“Inawezekana kukosekana kwake Cavani, Neymar na Mbappe kuliisaidia timu,” alisema kwenye kikao.

“Inawezekana msukumo ulikuwa chini sababu kila mtu alikuwa anashangaa tutashindaje bila wachezaji watatu muhimu,” aliongezea

Katika kundi A ,PSG inongoza jedwali kwa alama 3,Galatasaray alama 1,Club Brugge alama 1 na Real Madrid ya mwisho bila alama yoyote

About Author

3 thoughts on “Di Maria aisaidia PSG kuizima Real Madrid

  1. Hi , I do believe this is an excellent blog. I stumbled upon it on Yahoo , i will come back once again. Money and freedom is the best way to change, may you be rich and help other people.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *