Lampard atwikwa mikoba ya kuinoa klabu ya Chelsea

Klabu ya Chelsea imemteua aliyekuwa kiungo wao wa kati Frank Lampard kuwa kocha mkuu na kuchukua mahala pake Maurizio Sarri ambaye amekwisha tia sahihi kuinoa Juventus ya Italia.

Lampard amekua akiifunza klabu ya Derby County inayoshiriki ligi ya daraja la pili kule Uingereza mpaka alivyoteuliwa na Chelsea, Ametia sahihi mkataba wa miaka mitatu ya kuishi kule “Stamford Bridge”.

Katika historia yake Lampard akiichezea Chelsea kwa miaka 13 , alikuwa na mafanikio mengi kwa klabu akiwafungia mabao 211 kwa mechi 649 aliyocheza na kuwashindia mataji kadhaa.

Akizungumza na tovuti rasmi ya klabu Lampard alisema kwamba anafuraha Sana kurudi Chelsea Kama kocha mkuu.

“Najua kila mmoja anafahamu historia na upendo ninao kwa klabu,Lakini kwa sasa shabaha yangu kwa klabu kama kocha ni kujiandaa vyema kwa kipindi kjacho Cha ligi kuu Uingereza,” alisema kwenye mahojiano.

“Niko hapa kufanya kazi kwa bidii,Kuleta mafanikio mema kwa klabu na ninangoja kuanza kazi,.” Lampard alisema.

Kocha huyo mpya ataifunza Chelsea akisaidiwa na Jody Morris ambaye pia aliwahichezea klabu hiyo kama kiungo wa kati na Chris Jones ambaye atahudumu kama kocha wa timu ya kwanza.

Imeandikwa na Adams Kinanga
adams@wessay.co.ke

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *