Afisa mkuu mtendaji wa TSC (Kushoto) akiwa kando ya waziri wa elimu Profesa George Magoha (kulia) Pamoja na washikadau Picha kutoka Twitter kwa hisani

Walimu wanasababu ya kutabasamu baada ya tume ya kuwaajiri walimu nchini (TSC) kusema kuwa wamejadiliana na kampuni zinazotoa bima kwa walimu na kwamba watagharamiwa endapo watapatikana na virusi vya korona na kuwa itasaidia walimu kadri ya uwezo wao.


Afisa mkuu mtendaji wa tume ya walimu nchini (TSC) Nancy Macharia amewahakikishia walimu wenye miaka 58 na zaidi ambao wako na matatizo ya afya kuwa hawatofutwa kazi.


Akiongea baada ya mkutano na washikadau kwenye sekta ya elimu , Bi Nancy amesema walimu hao wameruhusiwa kufanya kazi wakiwa nyumbani na wanaweza kusaidiwa katika shughuli za kusahihisha mitihani.

Ametoa nambari 20207# itakayowasaidia walimu kuripoti visa vya corona au visa wanayoshuku kuwa korona kwa kampuni za bima itakayowasaidia kupata usaidizi kutoka kwao.


Bi Nancy aidha, amewashukuru walimu kwa juhudi zao haswa msimu huu wa korona,akifurahishwa na namna walimu wanavyoongoza wanafunzi kufwata kanuni za wizara ya afya za kudhibiti msambao wa virusi vya korona nchini.

Ratiba ya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane(KCPE) na kidato cha nne (KCSE) vilevile imezinduliwa mitihani hiyo ikitarajiwa kuanza machi mwakani.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *