Picha kwa hisani


Chama cha Madaktari nchini Kenya , KMPDU kimetishia kugoma ifikapo tarehe 6 Desemba, 2020 wakielezea kuupuzwa na serikali kuu.


Wakiongozwa na katibu mkuu wao Chibanzi Mwachonda, madaktari hao wamelalamikia mazingira magumu ya kufanyia kazi, wakieleza kuwa wahudumu wa afya 12 walipoteza maisha yao Jumatatu, Novemba 23, 2020.


Wametaka kupewa bima ya afya itakayojumuisha madaktari wote kwani madaktari wa kaunti , vyuo vikuu na wale wa mashirika ya serikali hawakujumuishwa kwenye bima ya afya kwa madaktari iliyozinduliwa hapo awali.

Madaktari hao wameitaka serikali kuu kutoa vifaa vya kujikinga dhidi ya corona (PPE’s) na kutaka kila serikali za kaunti kuajiri madaktari 50 watakaosaidia kupambana dhidi ya virusi vya corona, hospitalini.


Chama hicho kimesema kuwa madaktari wapatao 188 walioajiriwa mnamo Agosti , 2020 kwa kandarasi ya miezi sita na wizara ya afya kuhudumia wagonjwa wa corona, hawajalipwa mishahara yao hadi sasa na hawakupatiwa bima ya afya walipokuwa wakiajiriwa.

Wamegadhabishwa na hatua ya wizara ya afya kulazimisha madaktari hao kufanya kazi kwenye idara nyingine kwenye hospitali kwa kuwa kuna upungufu wa madaktari.


KMPDU imepuzilia mbali matamshi ya waziri wa afya Mutahi Kagwe kuwa madaktari wanaambukizwa virusi vya corona wakiwa nje ya hospitali.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *