Michael Olunga Kwenye Mechi

Mshambulizi wa timu ya taifa ‘Harambee Stars’ na anayechezea klabu ya
‘Kashiwa Reysol’ inayoshiriki ligi ya daraja la pili kule Japan, Michael Olunga, anatarajiwa kujiunga na timu ya taifa inayokita kambi jijini Paris, Ufaransa.Hi ni baada ya klabu hiyo kuafikiana na shirika linalosimamia soka humu nchini, (FKF).

Mchezaji huyo anawasili baada ya vuta ni kuvute kati ya FKF na klabu hiyo ambayo ilikuwa inataka kumwachilia Jumapili pindi mechi yao ya ugenini dhidi ya klabu ya Ehime FC kukamilika. FKF ilitaka Straika huyo kuingia kambini mapema ili kuisaidia timu katika safu ya Ushambulizi. Shirika la soka duniani FIFA iliingilia Kati na kutatua utata huo na Reysol wakakubali kumwachilia mchezaji huyo,FKF ilikuwa imetuma ombi kwa FIFA ikiiomba kuingilia Kati na kutatua swala hilo.

Olunga Mazoezini
Olunga akiwa katika Mazoezi, Picha kwa Hisani

Kikosi hicho kinachojumuisha wachezaji 27, chini ya kocha Mfaransa Sebastian Migne, watacheza mechi ya kirafiki na Madagascar Ijumaa, huko Paris, wanapoendelea kujinoa makali ili waweze kufanya vyema katika kundi C inayojumuisha, Senegal, Algeria na Taifa stars ya Tanzania katika kinyanganyiro cha kuwania ubingwa wa kombe la Mataifa barani Afrika(AFCON).

Wengine ambao wameingia kambini ni pamoja na , Erick Johana ,Erick Ouma ‘marcelo’ ,kipa Patrick Matasi miongoni mwa wachezaji wengine.

adams@wessay.co.ke

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *