Gavana Oparanya ahidi kukabiliana na visa vya ukosefu wa usalama Matungu

Wycliffe Oparanya

Picha kwa hisani ya Hivisasa

Gavana Oparanya alipatia swala la usalama kipau mbele kwenye hotuba yake katika sherehe za siku kuu ya Madaraka ,katika uwanja wa Bomani gatuzi dogo la Mumias magharibi.Akirejelea Visa vya utovu wa usalama vilivyotendeka kenye gatuzi dogo la Matungu ,alieleza kwamba atashirikiana na serikali kuu kuimarisha usalama eneo hilo.


“ Sisi Kama serikali ya gatuzi la Kakamega tukishirikiana na serikali kuu tutahakikisha kuwa jinsi tuwezavyo kusitisha matendo ya makundi haya haramu.Hawataepuka mkono wa sheria,” ananukuliwa kwenye hotuba yake.


Ikumbukwe kuwa eneo la Matungu limeshuhudia Visa vya mauaji ya watu kutoka kwa watu wazima Hadi watoto huku idadi ya vifo vikiripotiwa kufika taktibani watu 12 huku muathiriwa wa hivi karibuni akiwa mtoto wa miaka saba.


Sherehe ya Madaraka ilifaa kuandaliwa kwenye gatuzi dogo la Matungu lakini kwa sababu za operesheni ya kiusalama inayoendelea ikabidi igeuzwe na kuandaliwa Mumias .


Gavana aliomba umati kuchukua fursa kusimama na kunyamaza kwa kipindi kifupi ili kuwakumbuka jamaa waliopoteza maisha kufuatia visa vya utovu wa usalama kwenye eneo hilo.


Vilevile aliwatadharia wale wanaofadhili makundi hayo haramu.” Tungependa kutahadharisha wale wanaowaunga na kuwapa ufadhili wa kuendeleza maovu haya kuwa siku zao zimefikia kikomo.

okothj@wessay.co.ke

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *