Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Kakamega aomba serikali kuu kuongeza fedha katika afisi za wakilishi wa wanawake

Elsie Muhanda

Picha kwa hisani ya info.mzalendo.com

Kwenye hotuba yake kwa wananchi wa gatuzi la Kakamega katika sherehe za Madaraka, Elsie Muhanda aliomba serikali kuu kuongeza mgao wa fedha kwenye afisi za wakilishi wa wanawake ili kuwawezesha kufanikisha miradi yao mbalimbali ya maendeleo. Alijipigia debe utendakazi wake japo akisisitiza uhaba wa fedha kuwa kizingiti katika kufanikisha miradi mbalimbali katika kaunti hiyo.

Huku akiorodhesha miradi yake aliyoitekeleza akiwa mamlakani,alielezea kuwa afisi yake imepiga hatua kubwa kwa muda mchache tangu achukue hatamu Kama mwakilishi wa wanawake.

“Ndugu zangu wapendwa, ningependa kumjulisheni ya kwamba japo uchache wa pesa za kufadhili miradi mbalimbali .Afisi yangu imepiga hatua kadha muda mfupi ambao tumeweza kushirikiana na nyinyi kufanya kazi,” ananukuliwa kwenye hotuba yake.

Baadhi ya miradi yake kama ilivyoorodheshwa ni;

  • Kuwapa vijana mafunzo katika vyuo vya NITA
  • Kuwapa wanabodaboda mafunzo ya barabarani na baadaye kuwapa leseni
  • Kufadhili elimu ya wanafunzi mayatima kupitia mpango wa Eagle Scholarship
  • Kuwarudisha shuleni wasichana waliojifungua wakiwa shuleni kupitia mpango wa Tumaini Scholarship
  • Kufadhili ukulima kwa kuwapa wakulima walio na mapato ya chini mbolea pamoja na mbegu ili kuongeza chakula
  • Mradi wa maji ya visima katika eneo wadi sitini
  • Kuanzishwa kwa miradi ya  ‘Kakamega County Maendeleo Sacco’ ambao umewezesha wanachama kupata mkopo wa soko Loan na Bodaboda loan
  • Kufadhili miavuli kwa wanabiashara wenye mapato ya chini katika soko zetu
  • Kuwajengea nyumba wananchi walio na mapato ya chini
  • Kugawa fedha kwa makundi yaliyojisajili kihalali ili yaendeleze miradi yao

Vilevile  alipongeza viongozi wa gatuzi la Kakamega kwa kushirikiana vizuri katika kuleta maendeleo.

   okothj@wessay.co.ke

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *