Fainali za kombe la bara la Afrika, kung’oa nanga hii leo nchini Misri

Baada ya ngoja ngoja, sasa, kombe la mataifa la bara Afrika linang’oa nanga rasmi hii Leo nchini Misri.kikiwa ni kibute Cha 32 tangu kombe hili kuanzishwa mwaka wa 1957, Timu 24 ambazo zilifuzu kuingia fainali ya kombe hili,zimekusanyika kule Misri tayari kutifuana kwa kutafuta ushindi wa kombe hili.

Afrika mashariki kwa mara ya kwanza inawakilishwa na timu tatu ambazo ni Kenya, Tanzania na Burundi inayoshiriki kombe hili kwa mara ya kwanza ikijumuishwa ndani ya kundi B pamoja na Nigeria, Guinea na Madagascar ambayo pia inacheza kwa mara yake ya kwanza,Mauritania pia inashiriki kwa mara ya kwanza.

Hii Leo kumeratibiwa mechi moja ya ufunguzi ambako wenyeji Misri watafungua tafrija hiyo na na Zimbabwe mida ya saa tano usiku majira ya Afrika mashariki.

Hii ndio orodha ya makundi ya timu 24 zinazoshiriki dimba hili;

Kundi A
Misti ,Uganda,Zimbabwe,jamhuri ya kidemokrasia ya kongo

Kundi B
Nijiria,Gine,Burundi,Madagaska

Kundi C
Kenya,Aljeria,Senegali, Tanzania

Kundi D
Moroko,Afrika kusini,kodivaa,Namibia

Kundi E
Angola,Mali,Tunisia,Moritania

Kundi F
Kameruni,Benini,Ghana,Ginebisau

Imeandikwa na Adams Kinanga
adams@wessay.co.ke

About Author

1 thought on “Fainali za kombe la bara la Afrika, kung’oa nanga hii leo nchini Misri

  1. Amazing! This blog looks just like my old one! It’s on a completely different subject but it has pretty much the same layout and design. Outstanding choice of colors!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *