Wanafunzi wa KMTC kupokea chanjo ya AstraZeneca

Kutoka kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya KMTC Profesa Michael Kiptoo na Katibu mkuu mtendaji wa KMTC Profesa Philip Kitoko

Afisa mkuu mtendaji wa chuo cha mafunzo cha matibabu nchini KMTC Profesa Michael Kiptoo amedokeza wanafunzi wa mwaka wa 3 na 4 kutoka chuo hicho watapokea chanjo ya Astrazeneca kwa ushirikiano na serikali za Kaunti.


Akizungumza na vyombo vya habari kwenye hafla ya kusherehekea miaka 94 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho,Profesa Kiptoo amesema KMTC imepoteza wafanyakazi 4 kwa virusi vya korona. Aidha hakuna mwanafunzi yeyote aliyepoteza maisha yake kwa virusi hivyo.


Vilevile, amesema KMTC imeshirikiana na hospitali  karibu na vyuo hivyo kutoa matibabu kwa wanafunzi watakaoambukizwa na virusi hivyo.


Kwa upande wake, mwenyekiti wa bodi ya KMTC Profesa Philip kaloki amesifia utendakazi na mchango wa chuo hicho katika sekta ya afya.


“Kila mwaka KMTC hupeleka mahafala kwenye mpango wa serikali kuu ya kutoa afya bora kwa wakenya UHC ili kuziba pengo la upungufu wa wahudumu wa afya. Tangu 2013, mahafala takriban 60,649 wameingia kwenye mpango wa UHC,” akasema Profesa Kaloki.

Profesa Kaloki pia ameeleza mpango wa bodi ya KMTC kuongeza wahadhiri 150 kusaidia kwenye mafunzo ikizingatiwa idadi ya wanafunzi inaongezeka kila kuchao.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *