Viongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu kujumuishwa katika uundaji wa sera

Afisa mkuu mtendaji wa bodi wa uainishaji filamu nchini Ezekial Mutua amesema kuwa bodi hiyo inatafuta mbinu ya kushirikiana na viongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu katika  uundaji wa sera kuhusu uongozi wa taifa.

Akizungumza kwenye Kongamano iliyowaleta pamoja wadau kutoka bodi ya kupambana na ukeketaji,tume ya uwiano na maridhiano nchini pamoja na bodi ya uanishaji filamu, Mutua ameeleza kuwa wamechukua orodha yao na nambari zao ili kuwahusisha katika mambo uongozi na uundaji sera ikizingatiwa kuwa umri umewakubali na wanaweza saidia kupitisha ujumbe kwa kizazi cha sasa.

Ameeleza kuwa bodi yake inapanga kutumia viongozi wa vyuo vikuu kueneza ujumbe wa kutengeneza filamu safi zisikokuwa na maudhui ya ngono au ujumbe wa chuki.

Mutua amependekeza viongozi hao waandamane na viongozi serikalini wanapoenda ziara nchini za magharibi kubadilishana mbinu na mikakati  kwa madhumuni ya kupata maarifa zaidi kuhusu uongozi.

“Wako na nguvu na msisimko ikizingatiwa kuwa wao ni viongozi kwenye vyuo vikuu wala si shule ya msingi au upili,ni ishara tosha kuwa wanaezaleta mabadiliko nchini kupitia uongozi,” alisema Mutua.

Afisa mkuu mtendaji wa bodi ya kupambana na ukeketaji Bernadette Loloju ametaja kuwa viongozi wa wanafunzi katika vyuo vikuu wanamchango mkubwa katika vita dhidi ya ukeketaji akieleza kuwa wao ndio wazazi wa kesho na wanaweza zuia wanawao kutokeketwa siku zijazo.

Kwa upande mwingine,Olive Mutet afisa kutoka tume ya uwiano na utangamano ameeleza umuhimu wa vijana hao akitaja kuwa wao ni nguzo muhimu ya kujenga taifa na kwamba watasaidia kueneza ujumbe wa amani wakati ambapo nchi ikikaribu kuanda uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Bernard Karanja kiongozi wa wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Kenyatta amepongeza kongamano hilo akisema kuwa huu ndio wakati mwafaka wa kuleta vijana kwenye meza ya majadiliano na kuchangia katika ubunifu wa sera nchini.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *