Ufaransa na ujerumani wako ndani ya 16 bora na mechi moja mkononi
Timu ya wanawake ya Ufaransa na Ujerumani ndizo timu za kwanza kabisa kujikatia tiketi ya kuingia ndani ya 16 bora huku wakiwa na mechi moja mkononi katika dimba la dunia ya wanawake linaloendelea nchini Ufaransa.
Wenyeji wa dimba, Ufaransa, walianza vizuri safari yao ya ubingwa kwa kuifunga Korea kusini mabao 4-0 katika mechi ya ufunguzi tarehe 7 mwezi Juni, alafu jumatano ya wiki hii, waliipiga Norwe mabao 2-1 na kufunzu.

(Picha kwa hisani ya AFP :Getty images)
Mjerumani naye alishinda mechi zake mbili dhidi ya Uhispania tarehe 8 na Uchina tarehe 12 mtawaliwa ili kujipa nafasi katika 16 bora.

(Picha kwa hisani ya FIFA)
Australia ilitoka nyuma hiyo Jana na kuifunga Brazil mabao 3-2 jana, Brazil ilitangulia kufunga kwa dakika 28 kupitia kwa mkwaju wa penalti lililotiwa nyavuni na Straika Marta na kufunga bao la pili dakika 38 ,bao lililofungwa na Cristiane.
Foord Caitlin aliirudisha Australia kwenye mchezo kwa kuunganisha pasi yake kiungo wa kati Logarzo Chloe dakika 46 na kupatia Australia bao lake la kwanza.Katika dakika ya 58 ya mchezo, Chloe aliifungia Australia bado la pili, naye Mlinzi wa Brazil Monica alijifunga dakika ya 66 na kuisaidia Australia kushinda mechi hiyo kwa mabao 3-2.
Katika Mechi nyingine, Afrika Kusini ilipoteza mechi yake ya pili baada ya kunyukwa bao 1-0 na Uchina, Afrika Kusini ni ya mwisho katika kundi B bila alama zozote.
Ijumaa ya Leo kumeratibiwa kuchezwa michuano tatu Japan wakifungua uwanja na Scotland saa kumi jioni,Mida ya saa moja usiku Jamaica itashuka uwanjani kumenyana na Italia na Uingereza imalize udhia na Argentina saa nne usiku saa za Afrika mashariki.
Imeandikwa na Adams Kinanga
adams@wessay.co.ke.