Serikali yaombwa kufungua kivuko cha Ferry

Afisa anayeshughulikia masuala ya dharura katika shirika la Haki Africa Mathias Shipeta (Picha Kwa Hisani)

Shirika la kutetea haki za binadamu Haki Afrika limetoa wito kwa serikali kuruhusu kundi la kina mama wajawazito,walemavu na wazee kutumia kivuko cha Ferry.

Kupitia afisa anayeshughulikia masuala ya dharura Mathias Shipeta,shirika hilo limesema kundi hilo linapata changamoto kutumia daraja la Liwatoni wakilazimika kutembea kilomita nyingi.

“Walemavu,wajawazito na wazee wanapata shida. Daraja ni ndefu na kilomita nyingi kuivuka,”akasema Shipeta.

Shipeta amemtaka mshirikishi wa ukanda wa Pwani John Elungata kutoa agizo ya kufunguliwa kwa kivuko cha Ferry akisema itakuwa rahisi kwa kundi hilo na umma kutumia.

Kamati ya dharura ya kushughulikia Covid-19 ya kaunti ya Mombasa ilitoa agizo likita umma kutumia daraja la Liwatoni badala la kivuko cha Ferry, hatua hiyo ikidhamiriwa kudhibiti msambao wa Korona.

Hata hivyo,wanaotumia daraja hilo wameeleza kutofurahishwa na agizo hilo kwani kumeshuhudiwa msongamano mkubwa kwenye daraja hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *