Robert Alai akamatwa

Robert Alai amekatwa na kufikishwa katika makao makuu ya upelelezi .Mwanablogu huyo amekamatwa kwa madai ya kuchapisha picha za kutisha na zisizofurahisha ya mkasa ambao maafisa wa usalama walipoteza maisha yao kutokana na shambulizi linalokisiwa kutekelezwa na kundi la kigaidi la Al-Shaabab .Shambulizi hilo lililotekelezwa na kilipuzi liliwaua takribani maafisa Saba wa kulinda usalama.
Tume ya kitaifa ya uwiano na utangamano (NCIC) ilikashifu kitendo Cha Mwanablogu huyo na kumtaka azitoe picha hizo kwenye ukurasa wa mtandao wake wa jamii.Kupitia ujumbe kwa vyombo vya habari,tume hiyo ilisema kwamba ,kusambazwa kwa picha hizo zinaezaleta athari kwa familia ya waliopoteza wapendwa wao kwenye mkasa huo na kuhujumu umoja wa nchi.
“Tume hii inakashifu usambazaji wa hizi picha kwa maana inachukuliwa Kama kusifu vitendo vya kigaidi,” ujumbe huo unanukuu.
Watumizi wengine wa mitandao ya kijamii walitahadharishwa kutosambaza picha hizo .
“Tungependa kumtaka bwana Alai atoe picha hizo mara moja kutoka kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii na kurai watu wengine wanaotumia mitandao ya jamii kutosambaza picha hizo,” sehemu ya mwisho inanukuu hivyo.
Robert Alai alionekana kujitetea akisema kuwa ataendelea kuwatetea maafisa wa kulinda usalama ambao wamedhalilishwa na ada zao kuchukuliwa na ‘wakubwa’.Aliweka ujumbe huo kwa ukurasa wake wa Twitter.

Imeandikwa na John otieno
okothj@wessay.co.ke