Rashford aongeza mkataba wake na Manchester United

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Marcus Rashford ametia sahihi mkataba mpya wa kuichezea Machester United hadi mwaka wa 2023.

Marcus Rashford ambaye amewakilisha “mashetani wekundu” Kwa mechi 170 na kuwafungia mabao 45 amerefusha mkataba wake kwa miaka mitatu Zaidi na kuwaondolea hofu wamiliki na washikadau wote wa klabu hiyo.

Mshambulizi huyo ambaye pia amekulia katika akademia yao angetimukia klabu ya Barcelona pindi tu mkataba wake ungekamilika mwaka 2019-2020 kulingana na tetesi za vyombo vya habari nchini humo.

“Manchester United imekuwa kila kitu kwangu tangu kujiunga nao nikiwa na miaka Saba,Klabu imenitengeneza kuwa mtu na mchezaji mzuri na ni bahati Sana kila wakati nikipata nafasi ya kuvaa jezi yao.

“Nitafanya kila niwezalo kuisaidia klabu kurudi katika ubora wake na kuleta matokeo ambayo Mashabiki wanataka,” Rashford aliongea kwenye mahojiano na runinga ya timu hiyo.

Kwa mkataba huu mpya,Kinda huyo wa miaka 21 ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza atakuwa anatia kibindoni Kati ya pauni £200,000-300,000 kwa kila wiki .

kwa hilo donge nono Rashford amejiunga na wachezaji mastaa kama vile Alexis Sanchez, Paul Pogba, Romelu Lukaku wote wa Manchester United, Kevin De Bruyne wa Manchester City na Mesut Ozil wa klabu ya Arsenal wanaolipwa mshahara mnono katika ligi kuu ya Uingereza.

Kwa upande wake kocha Ole Gunnar Solskjaer alisema kwamba Marcus ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa Sana nchini Uingereza kwa wakati huu na amebarikiwa na kasi na nguvu nyingi.

“Marcus ni mfano mwema wa vipaji vinavyotoka kwa akademia yetu na ni kweli anafahamu ni nini maana ya kucheza Manchester United,” kocha Ole Gunnar ananukuliwa.

“Licha ya kwamba ana miaka 21, Rashford tayari ana uzoefu wa kucheza na ana maisha mazuri mbeleni Kama mchezaji, tunashukuru kwa kutia sahihi mkataba mpya,”kocha Solsjaer aliongezea.

Imeandikwa na Adams Kinanga
adams@wessay.co.ke

About Author

3 thoughts on “Rashford aongeza mkataba wake na Manchester United

  1. He has seen his future, because Lukaku is leaving and the central forward is remaining for him to make Man united stable, I like it@ Marcos#10

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *