Rais Samia Suluhu amteua Philip Mpango kuwa makamu rais

Makamu wa Rais mteule Philip Mpango (Picha Kwa Hisani)
Rais wa Tanzania Samia Suluhu amemteua Dkt Philip Mpango kuwa makamu rais akingoja kuidhinishwa na asilimia 50 ya bunge la taifa hilo kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.
Dkt Mpango amekuwa waziri wa fedha na mipango tangu Novemba 2015.
Awali alihudumu kama kaimu kamishna wa mamlaka ya ukusanyaji ushuru Tanzania TRA ,katibu mtendaji katibu afisi ya rais akisimamia tume ya mipango,Naibu katibu wa kudumu katika wizara ya fedha na uchumi na vilevile msaidizi wa kibinafsi wa rais katika masuala ya uchumi.
Pia amewahi hudumu kama mkuu wa kitengo cha kushauri rais kuhusu uchumi,mtaalamu wa uchumi mkuu katika benki ya dunia na mhadhiri wa uchumi wa umma katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.