Mwanafunzi wa chuo kikuu Cha sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro apatikana amefariki katika chumba chake

Marehemu Sydney ogeto

Hali ya huzuni imetanda katika chuo kikuu cha sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro baada ya mwili wa mwanafunzi wa mwaka wa nne anayesomea taaluma ya mazingira kupatikana amefariki kwenye nyumba anamoishi katika mtaa wa Jua kali, Kefinco viungani mwa mji wa Kakamega kwa njia ya kutatanisha.

kulingana na wanafunzi wenzake wanadai kuwa walimuona mwanafunzi huyo kwa jina Sydney Ogeto kwa mara ya mwisho siku ya ijumaa kabla ya kubomoa mlango uliokuwa umefungwa kwa ndani na kuupata mwili wake ukiwa kitandani.

Hata hivyo wanafunzi hao wa chuo hicho kupitia kwa kiongozi wao Vincent Simiyu Lumala wamekashfu kifo hicho na kutaka polisi kuanzisha uchunguzi wa kina wakidai kuwa sio kisa cha kwanza mwanafunzi wa chuo hicho kupatikana amefariki kwa njia ya kutatanishi wakisema kuwa miezi michache zilizopita wameshuhudia visa sawia na hicho.

Kamanda wa polisi Kakamega ya kati David Kabena amethibitisha kisa hicho na kusema kwamba uchunguzi wa kina tayari umeanzishwa.


About Author

3 thoughts on “Mwanafunzi wa chuo kikuu Cha sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro apatikana amefariki katika chumba chake

  1. Habari ya kutatanisha kweli,na ni tumai langu kuwa uchunguzi utafanywa ili kubaini kifo Cha mwanafunzi huyo,Maulana ailaze roho yake mahali pema peponi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *