Hadithi nawaleteya, garama sitoitisha  Miye mpenda umbeya, ndewe zenu nishabisha Udaku nimekoleya, na bado nitazidisha

Yule mke wa Tajiri, sidhani ana kifuli.


Msidhani nataniya, eti kuwa hana nywila Lango lake la bandiya, huliwacha yeye bila Watu wote huingiya, wa kurudi na kulala Yule mke wa Tajiri, sidhani ana kifuli.


Naona miye huruma, Kwa Tajiri aishipo Mjini alijituma, ajikite apatapo Iweje mkewe nyuma, kifuli chake hakipo? Yule mke wa Tajiri, sidhani ana kifuli.


Umbeya nakamilisha, kuwapasha yanojiri Maoni sitoitisha, kuhusu alonajiri Sitaki kumwaibisha, mke huyo wa tajiri Yule mke wa Tajiri, sidhani ana kifuli.


AGGREY BARASA 

 (Bongopevu)

About Author

1 thought on “Mkewe hana kifuli

  1. You actually make it seem really easy with your presentation but I in finding this matter to be really one thing that I feel I might by no means understand. It sort of feels too complicated and very large for me. I’m taking a look forward on your subsequent publish, I will try to get the cling of it!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *