Mchakato wa kubuniwa kwa chama cha Pwani yapigwa jeki

Mchakato wa kubuniwa kwa chama cha Pwani imepigwa jeki, raundi hii wakaazi wa Mombasa wakitoa shinikizo hilo wakisema Pwani imekosa sauti moja halkadhalika hapajakuwa na  uwakilishi dhabiti ndani ya vyama vinavyodai kuwawakilisha.

Kupitia mwakilishi wao Francisca Kitese,wakaazi hao wamesema kuwa chama hicho kitapigania masuala ya wapwani ikiwemo usawa na uwakilishi bora bungeni na vitongojini.

Vilevile wametaka chama hicho kujumuisha kikamilifu ‘wabara’ ikizingatia wanamchango mkubwa kwa kukua kwa Pwani kiuchumi,kisiasa na kijamii.

“Utafiti unaonyesha kabila kubwa Pwani ni wakamba ikifuatwa na mijikenda,waluhya,wajaluo,Gema na waswahili.Inasikitisha kuona hakuna mbunge kutoka jamii ya waluhya au Gema,” akasema Kitese.

Wameongezea kuwa wataungana na waanzilishi wa chama hicho na kukisaidia katika shughuli zake ili kuipa Pwani sura mpya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *