Marekani yainyamazisha Thailand kwa kuifunga mabao 13-0

Picha kwa hisani ya FIFA Women World Cup
Bingwa mtetezi wa kombe la dunia ya wanawake mwaka wa 2015 Marekani hiyo Jana alionyesha hamu na uwezo wa wakutetea taji lao kwa kuifunga na kuinyamazisha timu ya taifa ya Thailand kwa kichapo Cha mabao 13-0.
Straika wa klabu ya Orlando pride ya wanawake aliifungia Marekani mabao matano ,naye kiungo wa Kati Levelle Rosa,straika Pugh Mallbry na Lloyd Carli wa klabu ya sky blue ya wanawake walicheka na nyavu mara mbili Kila mmoja kwa faida ya Marekani.
Kiungo wa Kati Rapinoe Megan na mvamizi Press Christian waliizima Thailand kabisa kwa kufunga mawili ya mwisho na kuihakikishia mabingwa hao watetezi ushindi mnono katika kundi lao.
Katika nyuga zingine Uholanzi ilifunga Nyuzilandi bao bila jibu kwa hisani ya Roord Jill anayesakata soka na klabu ya Bayern Munich ya wanawake.Uswidi walijipatia alama tatu muhimu kwa kuifunga Chile mabao mawili kwa sufuri, mshambulizi Asllani Kosovare akifunga dakika ya 83 na Janogy Madelen akifunga goli la mwisho katika dakika ya 95.
Ratiba ya Leo mechi tatu zitachezwa Nigeria wakipiga na Korea kusini saa kumi, Ujerumani wafaane na Uhispania saa moja usiku na Ufaransa wamalize udhia na Norwe saa nne usiku majira ya Afrika mashariki.
Imeandikwa na Adams Kinanga
adams@wessay.co.ke.