Mabao matatu yake Cristiane yaiakikishia Brazil Ushindi

Picha kwa hisani

Kule Ufaransa kumewaka Moto. dimba la kombe la dunia ya wanawake linashika Kasi kweli,Hapo Jana kulichezwa mechi tatu ambako Australia walifaana na Italia,Brazili wakakipiga na Jamaica na Uingereza wakagaragazana na Uskochi.

Mshambulizi wa Brazil Cristiane hapo Jana alifunga mabao matatu kwa mechi yao na timu ya Jamaica na kuiakikishia timu yake ushindi muhimu wa kwanza katika kundi C.Malkia huyo wa miaka 34 ambaye pia anapiga soka ya kulipwa na klabu ya Paris saint German ya wanawake alifungua ukurasa wa magoli dakika ya 15 kwenye Kipindi Cha kwanza kupitia usaidizi wake kiungo wa Kati Alves Andressa.

Mnamo dakika ya 38 Alves Andressa alipoteza penalti lakini akajibu kwa kumuandalia Cristiane pasi na kufunga bao lao la pili dakika ya 50.Strika huyo alizima matumaini ya Jamaica ya kurudi mchezoni na bao lake la tatu katika dakika ya 64 na kuondoka uwanjani nafasi yake ikichukuliwa na Lodmila. Mechi hiyo iliisha 3-0 kwa faida ya Brazil.

Kwengineko Australia ilidhalilishwa na Italia kwa kufungwa 1-2.Mabao ya Italia yalifungwa na Benansea Barbara katika dakika ya 56 na 95. Australia walitangulia kufunga kupitia mchezaji Kerr Samantha katika dakika ya 22 kwenye Kipindi Cha kwanza.

Uingereza ama “The Lionesses” waliirindima Uskochi 2-1 kwa hisani ya Parris Nikita katika dakika ya 14 kupitia mkwaju wa penalty na White Ellen akafunga dakika ya 40 naye Emslie Claire akaifungia Uskochi katika dakika ya 79.

Hii Leo kumeratibiwa mechi mbili,Argentina wataikalibisha Japan saa moja usiku naye Kameruni Mwakilishi mwingine wa Afrika watakipiga na Canada mida ya saa nne usiku majira ya Afrika mashariki.

Imeandikwa na Adams Kinanga
adams@wessay.co.ke

About Author

1 thought on “Mabao matatu yake Cristiane yaiakikishia Brazil Ushindi

  1. I found your weblog site on google and check just a few of your early posts. Continue to maintain up the excellent operate. I simply extra up your RSS feed to my MSN News Reader. Looking for ahead to studying extra from you in a while!…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *