Kwaheri Ken Walibora

Wakili niko langoni, leyo tena nimefika
Siji nayo burudani, machozi yatiririka
Naomba nisikieni, nieleze yalotufika
Mola amlaze pema, Walibora katuaga
Hatari barabarani, furaha tena hatuna
Utovu huku mijini, imekua nyingi sana
Dereva bila leseni, mijini mejazana
Mola amlaze pema, Walibora katuaga
Kilio changu cha haki, zumbukuku kanishika
Kifo nitakusitaki, uzoefu sitotaka
Uchungu katamalaki, nitasema nikitaka
Mola amlaze pema, Walibora katuaga
Mashairi katutungia, ugwiji umesheheni
Riwaya katuandikia, isomwe humu shuleni
Studioni kaingia, mhafidhina makini
Mola amlaze pema , Walibora katuaga
Wenzangu nawaeleza , yalotupata jamani
Saa kumi ikianza , ni nyakati za jioni
Walibora aliweza , kutuaga buriani
Mola amlaze pema , Walibora katuaga
Wanafunzi sikieni , penye nia pana njia
Masomo zingatieni , ulegevu kufifia
Usingizi sitieni , vitabuni kipitia
Mola amlaze pema , Walibora katuaga
Wasikizi kwaherini , nimefika ukingoni
Watakao aniwani , wakili mie nyumbani
Nilosema kumbukeni , mkifika majumbani
Mola amlaze pema , Walibora katuaga
By Samson Odhiambo