KOMBE LA DUNIA YA WANAWAKE LANG’OA NANG’A NCHINI UFARANSA

Picha kwa hisani ya Fox sports

Kombe la dunia kwa upande wa kina dada mwaka 2019 limeng’oa nang’a nchini Ufaransa, Michuano hii inayoshirikiza timu 24 ilianza tarahe 7 mwezi huu na itatamatika tarehe 7 mwezi Julai.

Ufaransa ilifungua kibute hicho kwa kuititima Korea kusini mabao 4-0,mabao yao yalikifungwa na Le Sommer dakika ya 9 wa mchezo,Renard Wendie dakika 35 na 47 na kiungo wa Kati Henry Amandine akiifungia Ufaransa bao la mwisho katika dakika za lala salama na kuihakikishia ushindi huo muhimu.

Kwenye mechi za hapo awli wajerumani waliwabwaga wenzao wa china kwa bao moja kwa nunge (1-0),Uhispania ikiilaza Africana Kusini mabao watatu kwa moja (3-1) na hatimaye Norwe ikaipatia adhabu Nigeria kwa kuwachabanga magoli matatu bila jibu (3-0).

Ratiba ya Leo kule Ufaransa ni kwamba Australia wataminyana na italia saa nane alasiri,Brazil wapimane nguvu na Jamaica saa kumi na nusu jioni kasha Uingereza wamalize udhia na Uskochi mida ya saa moja susiku majira ya Afrika mashariki.

Katika Michuano hii Bara la Afrika linawakilishwa na Nigeria,Kameruni pamoja na Afrika ya kusini.

Hi hapa ni orodha ya makundi ya timu 24 zinazoshiriki dimba hili;

Kundi A Kundi B Kundi C Kundi D Kundi E kundi F
Ufaransa Ujerumani Australia Uingereza kanada Marekani
Nigeria. Uchina Italia. Japani Kameruni Chile
Norwe Uhipania. Brazil. Argentina. Nyuzilandi Uswidi
Korea kusini. Afrika kusini. Jamaica. Uskochi. Uholanzi Thailand

Imeandikwa na Adams Kinanga
adams@wessay.co.ke

About Author

1 thought on “KOMBE LA DUNIA YA WANAWAKE LANG’OA NANG’A NCHINI UFARANSA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *