Kikosi cha Migne kitakachowakilisha Kenya kule Misri chatajwa

Picha kwa hisani ya FKF

Baada ya kuisaidia timu ya taifa “Harambee stars” kufunzu kucheza katika dimba la AFCON ambapo Kenya ilishiriki mwisho mwaka wa 2004 kwa kuifunga Ghana na Ethiopia nyumbani na vilevile kutoka sare ya kutofungana ugenini Addis Ababa Uhabeshi na kupoteza ugenini dhidi ya “The black stars” ya Ghana, kocha wa Harambee stars Sebastian Migne ameteua kikosi kitakachowakilisha Kenya kule Misri.

Christopher Mbamba, Clifton Miheso, Anthony Akumu na mlinzi wa Maritzbury Brian Mandela wamewachwa nje ya kikosi hicho na kocha Sebastian Migne, Mandela na Mbamba walichujwa nje ya kikosi Cha stars kwa sababu ya jeraha walizopata wakiwa mazoezini Ufaransa.

Kikosi hicho Cha wachezaji 23 Kinaongozwa na kiungo wa Kati wa Tottenham Victor Wanyama Kama kinara wao ,mchazaji anayecheza soka ya kulipwa Uingereza na mshambulizi wa Kashiwa Reysol ya Japan Michael Olunga waliokuwa nguzo muhimu kwa timu katika safari yao ya kufunzu kucheza kipute hicho.

Hichi ndicho kikosi Cha watu 23 kitakachosafiri na kocha Sebastian Migne kwenda Misri;

Patrick Matasi- kipa (saint Georges) Uhabeshi
John Oyemba – kipa (Kariobangi sharks)Kenya
Faruk Shikulo- kipa (Bandari) Kenya
Bernard Ochieng- Mlinzi (Vihiga United) Kenya
Abud Omar- Mlinzi (SEPSI OSK) Romania
Joseph Okumu- Mlinzi (Real Monarchs)U.S.A
Erick Ouma- Mlinzi (Vasalund) uswidi
David Owino- Mlinzi (Zesco) Zambia
Michael Olunga- Straika (Kashiwa Reysol) Japan
Dennis Odhiambo- Kiungo wa kati (Sofapaka) Kenya
Musa Mohammed- Mlinzi (Nkana) Zambia
Joash Onyango- Mlinzi (Gor mahia) Kenya
Johanna Omollo- Kiungo wa Kati (Cercle brugge) Ubeligiji
Masud Juma- straika (AL-Nasr Bengazi) Libya
Philemon Otieno- Mlinzi (Gor mahia)Kenya
Ismael Gonzalez- Kiungo wa Kati (Las Palmas) Uhispania
Ayub Timbe- Kiungo wa Kati (Beijing Renhe) Uchina
Victor Wanyama- Kiungo wa kati (Tottenham) Uingereza
Erick Johanna – Kiungo wa kati (IF Brommapojkarma) uswidi
Ovella Ochieng – Straika (Vasalund) Uswidi
Francis Kahata – Kiungo wa Kati (Gor mahia) Kenya
John Ovire – Strika (Sofapaka) Kenya
Paul Were – Kiungo wa Kati (AFC Leopards) Kenya.

Jumamosi hii “Harambee stars” itajinoa makali na timu ya kitaifa ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kule Uhispania kabla ya kuelekea Misri tarehe 19 na tarehe 23 washuke uwanjani kucheza mechi yao ya kwanza ya dimba hilo na Algeria mida ya saa tano usiku majira ya Afrika mashariki.

Imeandikwa na Adams Kinanga
adams@wessay.co.ke.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *