Joho azindua programu ya roboti kwa wanafunzi wa chekechea

Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amezindua mradi wa roboti kwa wanafunzi wa chekechea katika shule ya chekechea ya Buxton,mradi huo ukitarajiwa kusaidia wanafunzi hao katika masomo yao.

Joho amesifia programu hiyo akisema wanafunzi wa chekechea wataweza kutumia kompyuta kujifunza mambo kadha kuhusu teknolojia,kuinua viwango vyao vya uvumbuzi na kubadilisha maisha yao.

Ameongezea kuwa kutumia roboti kutawasisimua wanafunzi hao na kuwapa ari ya kurudi shuleni siku inayofuata, akisema kuwa wanafunzi hao watakua wakijua teknolojia ndio mkondo wa kufuata.

Awamu ya kwanza wa mradi huo utakuwa kwenye shule 20 nyingine zikitarajiwa kufuata na kila shule itakabidhiwa vipakatalishi 2 kusaidia kufunza program hiyo.

Gavana Joho amedokeza kuwa serikali yake inapanga kubadilisha chuo cha kiufundi moja kwenye kaunti hii na kuifanya kitovu cha teknolojia.

Aidha,amepuzilia mbali mjadala wa ‘wilbaro’ akisema kuwa inatukumbusha jinsi tulivyo maskini badala yake ametaka serikali kuu kutafuta namna ya kusaidia na kuwekeza kwa vijana.

“Takriban asilimia 10 ya bajeti ya taifa yafaa idhamirie jinsi itakavyosaidia vijana,kuwafanya wawe wafanyibiashara na kuwekeza katika maeneo yatakayowajenga na kuwaimarisha ili kuwe na maendeleo katika maisha yao,” akasema Gavana Joho

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *