Janga la korona

Jinamizi la korona, limetikisa dunia,
Adinasi kila moja , ugonjwa unawapata,
Watu kote ‘mepoteza, maishae kwa korona,
Korona hatari sana, haibagui kabisa,
Sote twaweza epuka, ‘kishikamana pamoja,
Kwa mikononi kunawa, mikutano kuepuka,
Kusimama mita moja, korona epuka sana,
Korona hatari sana, haibagui kabisa,
Tukae nyumbani waja, wadogoe kwa wakubwa,
Serikali navyosema, tuilinde yetu afya,
Tuikinge familiya, kutokana na korona,
Korona hatari sana, haibagui kabisa,
Tunapopiga chafiya, shashi ni chombo tumika,
Umoja wetu wakenya , tashinda hili janga,
Tamati nakamilisha, kudura zinatutosha,
Korona hatari sana, haibagui kabisa
©Kiptoo K. Edwin