Hatujatelekeza madaktari asema Mwangangi

Katibu Mkuu Mwandamizi Katika Wizara Ya Afya Nchini Kenya Mercy Mwangangi Picha Kwa Hisani

Katibu mkuu mwandamizi katika wizara ya Afya nchini Kenya Mercy Mwangangi amesema serikali haijawatelekeza madaktari nchini humu.


Mwangangi amesema kuwa madaktari ni muhimu katika vita dhidi ya virusi vya corona, akieleza kuwa serikali kuu inafanya kazi kwa ukaribu na serikali za kaunti kuhakikisha maswala yao yanatatuliwa.


Ameongeza kuwa yapo majadiliano kati ya wawakilishi wa vyama vya wahudumu wa afya na hazima ya bima ya afya nchini humo NHIF yatakayohakikisha shida zao zinatatuliwa.


Katibu huyo, amezungumza hayo alipotoa ripoti ya kila siku kuhusu maambukizi ya corona ambapo wakenya 727 wapya wameambukizwa virusi hivyo kutoka kwa sampuli 4,913 zilizopimwa huku watu 17 wakiaga dunia.

Watu 806 wamepona miongoni mwao 701 wamekuwa wakitibiwa wakiwa nyumbani ilhali wengine 105 wameruhusiwa kwenda nyumba.


Watu 1,196 bado wamelazwa hospitalini wakiugua corona, wengine 7,139 wakitibiwa wakiwa nyumbani.

Kauli ya Mwangangi inajiri wakati ambapo madaktari nchini Kenya, Jumanne Novemba 24,2020, walikuwa wametishia kuanza mgomo wao ifikapo tarehe 7 Desemba, 2020 endapo wizara ya afya haitotatua malalamishi yao yakiwemo mazingira magumu ya kufanyia kazi huku wakitaka wapewe bima ya Afya kwa madaktari wote nchini humo.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *