Buriani Muhammed Juma Njuguna

Picha kwa hisani

Tasnia ya uhanahabari inaomboleza kifo cha mkongwe Muhammed Juma Njuguna wa kituo cha redio Citizen kinachosimamiwa na shirika la Royal Media Services.Muhammed Juma Njuguna alifariki jana asubuhi baada ya kuugua kwa muda mrefu na kulazwa Nairobi hospital.Alikuwa amelazwa kwa muda wa wiki tatu zilizopita.
Mwanahabari huyo alijiunga na kituo cha redio Citizen mwaka wa 1999 kutoka KBC ambako amekuwa akihudumu kama mwanahabari wa spoti kwa miaka arubaini hadi kifo chake .Atakumbukwa sana kwa kuwa miongoni mwa wanahabari wa kwanza kuanza kutangaza mpira wa soka .Ueledi wake ulimfanya kutuzwa na rais mtaafu Mwai Kibaki tarehe 10 mwaka wa 2010.
Rais Uhuru Kenyatta aliongoza wakenya katika kutoa risala za rambirambi .Kwenye ujumbe wake ,rais alimtaja kama mwanahabari shupavu ambaye alitumia taaluma yake kufahamisha na kuburudisha wakenya hususan matangazo yake ya mpira wa kandanda.
“tumejawa na huzuni kwa kumpoteza mwenzetu.Muhammed alikuwa mwanahabari hodari .Alikuwa mzuri na kielelezo kizuri kwa tasnia ya uhanahabari na vilevile mtu wa kupigiwa mfano kwa wanahabari wanaokua ,” rais aliomboleza
“Wakati huu wa dhiki,mawazo yetu na maombi yetu yako na ndugu ,marafiki na familia ya mwendazake,”aliongezea
Naibu wa rais pia alituma ujumbe wake . “Muhammed Juma Njuguna mwanahabari aliyekolea alikuwa mwerevu na tena mchangamfu .Alifanya wengi wasikize redio kupitia uzoefu wake wa kutangaza mpira kwa ucheshi na kusisimua,”ananukuliwa.
Wakenya kupitia mtandao wa twitter walimtilia sifa chungu nzima kupitia kwa alama ya reli Muhammed Juma Njuguna.Wengi walisema watakosa sauti yake ilyowafanya kupenda matangazo ya kabumbu.Aidha wengine walitoa ujumbe wa kuifariji familia nakuwatakia mema hata wanapopitia wakati mgumu .
Imeandikwa na John Otieno
okothj@wessay.co.ke

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *